KARIBU SANA

Tuesday, 23 September 2014

JK AKIWA NEW YORK MAREKANI 


 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
  President Jakaya Mrisho Kikwete invites  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete bids farewell to Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
  President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete greets American civil rights activist and Baptist minister  Rev. Jesse Louis Jackson, Sr during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Mama Graca Machel when they met in Washington DC
 President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York
 President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York.STATE HOUSE PHOTOS

TPDC YAKANUSHA TAARIFA ZA UWONGO

                                                                               
Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa:  " Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. 

Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira  moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!...Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014".

TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

BWM Pensions Towers, Tower A,
Junction of Azikiwe /Jamhuri Streets
P. O. Box 2774,
Tel: +255 22 2200103/4
Dar-es-Salaam, Tanzania

  MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI ARUSHA LEO.

 Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini, Pereira Ame Silima. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza leo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo.

Kipanya


TAZAMA PICHA NA TAARIFA YA CHADEMA KUFANYA MAANDAMANO

  Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akimkaribisha Kigaila kuzungumza na wanahabari.
  Mwanasheria wa Chadema, John Malya akifafanua baadhi ya vipengere vya sheria kuhusu ruhusa ya kufanya maandamano.
  Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila akionesha barua za kuomba vibali vya kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.
  Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

MKUU:WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA MADAKTARI WA KUJITOLEA TOKA UJERUMANI MJINI SUMBAWANGA

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu  Pinda akiwa amepiga magoti wakati alipowasalimia wakwe baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri Mkuu, Kibaoni mkoani Katavi  Septemba 20, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Madaktari  kutoka Ujerumani ambao wako kwa muda katika Hospitali ya Kristo Mfalme ya Mjini Sumbawanha ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki. Madaktari hao wa kujitolea wanatibu magonjwa mbalimbali na kufanya upasuaji bure hospitalini hapo.  Kulia ni Askofu wa jimbo la Sumbawanga, Damian Kyaruzi.Mheshimiwa Pinda alifanya ziara hospitalini hapo Septemba 21, 2014.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Mfuko wa Pensheni (PSPF) umedhamini siku ya Msanii Tanazania itayoadhimishwa Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi  
---
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
 
Mfuko wa Pensheni (PSPF) umedhamini siku ya Msanii Tanazania itayoadhimishwa Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City kwa dhumuni la kuwapa mafunzo wasanii ili waweze kujikwamua kiuchumi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi amesema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Sanaa ni kazi” ambayo itajumisha fani mbalimbali kama vile Taarabu, Muziki wa dansi, ngoma za asili na muziki wa msanii kutoka nje ya nchi.

PICHA:ONA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA NA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI NAPE NNAUYE CHALINZE

   Jengo la zamani la Kituo kidogo cha Polisi Mbwewe.
   Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiingia kwenye jengo la Kituo cha Polisi Mbwewe kuzindua ujenzi wa kituo hicho leo, Septemba 22, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo la Chalinze  mkoa wa Pwani.
   Katibu Mkuu wa CCM Kinana akichapia kushiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi Miono
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) "akimsimamia' Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, wakati akichapia jengo la Kituo cha Polisi Miono, jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofsi ya CCM Kaya  ya Kiwangwa, jimbo la Chalinze. Pembeni yake ni Kinana akishuhudia




 Mitambo Miwili iliyofungwa katika kituo cha KINYEREZI ONE yenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 150 za umeme utakaogawanywa katika sehemu mbili kuingia katika gridi ya Taifa, ikiwa ni kujenga msongo wa kilovolt 220 kwenda Kimara na kujenga laini ya msongo wa kilovolt 132 kwenda Gongo la Mboto, Kituo hiki kitagharimu Dola za Kimarekani Milioni 183.
 Baadhi ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.
  Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme ili kuhakikisha wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa Ziara kwenye Mradi wa “Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)”  unaotekelezwa katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa habari kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza katika jitihada za kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.

  MKUU WA MKOA ARUSHA ALIPOZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA JIJINI ARUSHA

 Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Mpira wa Amri Abeid jijini Arusha jana. Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
 Waendesha pikipiki (bodaboda) pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha Amri Abeid, jijini Arusha jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”.
 Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Mkaguzi Msaidizi, Yohana Mjema (kulia), akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo (watatu kushoto), namna ajali barabarani zinavyoweza kuepukika endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani. Mkuu wa Mkoa aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira Amri Abeid jijini Arusha jana. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamedi Mpinga.

FROM THE STATE HOUSE:PRESIDENT JAKAYA KIKWETE SPEAKS ON CLIMATE CHANGE IN NEW YORK

 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his opening remarks during a meeting of the Committee of African Heads of State and Government on Climate change(CAHOSCC) held today at the office of the Permanent Observer Mission of the African Union(AU) to the United Nations in New York. On the right is the Chairperson  of the African Union Commission Dr. Nkosazana Dlamini Zuma. In his remarks,President Kikwete who is also the Coordinator of CAHOSCC reiterated his call on the need for Africa to speak with one voice in advancing and championing the continent’s common position and interests on Climate Change.
Delegates who attended the session on Climate Change in New York. Photo by Freddy Maro-State House

TaSUBa YAASWA KUTOA MAFUNZO YA SANAA NA UTAMADUNI IILI KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI

 Benjamin Sawe, Bagamoyo
--
Taasisi ya Sanaa Bagamoyo imeaswa kuendelea kutoa mafunzo ya sanaa na utamaduni  ambayo yatakidhi mahitaji ya soko  kwa nchi za Afrika Mashariki. 
Hayo yamesemwa na Bw Makongoro Nyerere kwa niaba ya  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margaret Ntantongo Zziwa katika Ufunguzi wa Tamasha la 33 la sanaa na utamaduni wa Mtanzania lililofanyika katika Taasisi hiyo mjini Bagamoyo jana
 
Bwana Makongoro alisema Sanaa na Utamaduni vinaweza  kutumiwa kuelezea masuala yote  yanayomuhusu binadamu na mazingira yake hususani suala zima la utaliii

VIDEO:Taarifa ya Habari Kutoka ITV: Bunge maalum la katiba limetoa azimio la kufanya marekebisho ya kanuni za bunge hilo ili kuweza kutoa ruhusa kwa baadhi wajumbe kuweza kupiga kura nje ya ukumbi wa bunge azimio ambalo limeibua mvutano kwa baadhi ya wabunge wakilipinga na kusema mfumo huo unaweza kutoa mwanya wa uchakachuliwaji kwa kura.

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA ELIMU: KUWAWEZESHA VIJANA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KIAFYA BARANI AFRIKA


 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014

SHIRIKA LA NYUMBA LATOA MASHINE 28 ZA KUFYATULIA MATOFALI KWA VIJANA MKOANI PWANI


 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani.Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment