Mwanasheria
IPTL/PAP asema hawhusiki na
fedha
za Profesa Tibaijuka
Prof. Anna Tibaijuka - Waziri.
SIRI
zaidi imezidi kufichuka kuhusiana na sakata la akaunti ya ESCROW na IPTL,
ambapo sasa imefahamika malipo yaliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari
kwamba Profesa Anna Tibaijuka alipewa fedha zinazotokana na akaunti hiyo sio
kweli, imefahamika.
Pia,
inadaiwa fedha hiyo zaidi ya sh. Bilioni 1.6 alizopata Profesa Tibaijuka kutoka
kwa mmoja waliokuwa wanahisa wa Kampuni ya kufua umeme ya Independet Power
Supply Limited (IPTL), James Rugemalila hazihusiani na akaunti hiyo.
Taarifa
zaidi za kuaminika kutoka katika ofisi za IPTL/PAP zilieleza kuwa fedha hizo
zilikuwa ni mali ya Rugemalila, ambaye wakati anatoa hizo fedha kwa Tibaijuka hakuwa
tena mwanahisa wa IPTL.
Ilisema
nyaraka zinaonyesha kwamba, Rugemalila alikwisha uza hisa zake zote alizokuwa
anamiliki kupitia kampuni yake ya VIP, ambapo alikuwa anamiliki asilimia 30 na
kuziuza kwa Kampuni ya PAP.
Akizungumza
kuhusiana na tuhuma hizo, Mwanasheria na Katibu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege
alisema katika suala nzima la IPTL ukweli unafichwa na umma hauelezwi.
Alisema
tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kueleza ukweli halisi, lakini umekuwa
ukipotoshwa kwa maslahi binfasi ya watu.
‘Rugemalila(VIP)
aliuza hisa zake zote na kufuata taratibu za kisheria na nyaraka zipo ofisini
kwetu na BRELA. Rugemalila hakulipwa fedha za ESCROW, bali alilipwa fedha za
kuuza hisa zake,’’alisema.
Makandege
aliongeza ‘Mtu mwenye fedha zake kaamua kumpa mtu mwingine ama kwa kumkopesha,
kumsaidia au kwa mapenzi yake mwenyewe fedha zake shida iko wapi na IPTL
inahusikaje hapa. Nafikiri Rugemalila ndiye anayejua matumizi ya fedha zake,’’.
‘Izingatiwe
kwamba fedha za ESCROW sio hisani wala rushwa ni malipo halali yanayotokana na
IPTL kuwauzia TANESCO umeme, ambao watanzania wameutumia na wanaendelea
kuutumia. Je, wanasiasa walitaka tuwape umeme bure,’’alisema.
Makandege
alisema IPTL/PAP ni mmiliki halali aliyefuata taratibu zote na malipo aliopewa
kutoka akaunti ya ESCROW ni halali na hakuna vitendo vya ufisadi vyovyote.
‘Umma
utakuja kuelewa katika suala hili, wanaozungumza wanatumiwa kwa kuwa IPTL/PAP
ndio kampuni inayoiuzia umeme kwa bei nafuu Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO)
kuliko kampuni zote na kinachofanyika ni wivu wa kibiashara,’’alisema.
Hivyo,
alisema IPTL/PAP haihusiki na fedha zozote alizopewa Profesa Tibaijuka, ambaye
ni Waziri wa Ardhi, Maendeleo na Makazi pamoja na watu wengine wote ikiwa wapo
wamepewa na watanzania waepukane na upotoshaji huo.
No comments:
Post a Comment