Hali imezidi kuwa mbaya na wingu kuzidi kuwa zito na jeusi kwa FREEMAN MBOWE na Dkt. SLAA baada ya kijana anayeaminiwa kuzijua na kuzifahamu njama zao za MAUAJI ya aliyekuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA CHACHA ZAKAYO WANGWE 28.7.2008 PANDAMBILI DODOMA Bw. DEUS FRANCIS MALLYA kutaka kujitokeza hadharani na kusema kila kitu na njama zilivyokuwa mpaka WANGWE alipouawa.
huu hapa chini ni ujumbe aliouandika MALLYA katika mtandao wa JAMII FORUMS mapema leo.
MALLYA anatarajiwa kuzungumza na watanzania hivi karibuni ili kueleza kila kitu kilivyokuwa.
stay tuned
mtandao huu unakuahidi kukuletea kila kitu.
Wakati wa mimi kusema umefika
Salaam!
Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali.
Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!.
Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'
Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake
Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.
Deus Mallya
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment