KARIBU SANA

Tuesday 16 September 2014

MCHEZO MCHAFU DHIDI YA IPTL WABAINIKA!



Wanajamvi baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwenye sakata linaloendelea dhidi ya kampuni ya IPTL, na TANESCO ukweli umebainika kuwa ni tofauti na watanzania wengi wanavyofikiria na kujikita kulijadili sakata hili kwa mahaba bila kujikita kuutafuta ukweli juu ya sakata hili.

MCHEZO MZIMA HUU HAPA 

Historia fupi ya iptl

IPTL ilianzishwa kwa Makubaliano kati ya Serikali na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha MW 100, yalifikiwa ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa umeme katika miaka ya 90. Serikali ilialika sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa vile haikuwa na fedha za kugharimia miradi ya umeme. Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd ya Tanzania (VIP) iliweza kuishawishi Serikali kualika Kampuni ya Mechmar Corporation ya Malasyia (MECHMAR), na baada ya MECHMAR kuonyesha kuwa inaweza kuzalisha MW 100 katika mji wa Dar es Salaam ilisaini MoU na Serikali. Mwaka 1994 Kampuni ya MECHMAR na Kampuni ya VIP kwa pamoja zilianzisha Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kama kampuni binafsi iliyokuwa inamilikiwa na MECHMAR kwa asilimia 70 na VIP kwa asilimia 30. Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga, kumiliki na kuendesha (Build-Own-Operate) mtambo wa kuzalisha MW 100 za umeme wa mafuta mazito katika eneo la Tegeta-Salasala. 

sababu ya kufunguliwa akaunti ya Escrow.
Akaunti ya Escrow ilifunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania baada ya Mkataba wa Escrow kusainiwa na Serikali (kwa niaba ya TANESCO), Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Benki Kuu ya Tanzania, tarehe 5 Julai, 2006.
Kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow kulitokana na ushauri wa Mkono and & Co. Advocates in association with Denton Wilde Sapte wa tarehe 30 Juni, 2004.

Ni vizuri ikaeleweka kuwa, akaunti ya Escrow ilifunguliwa kutokana na “Dispute” iliyotolewa na TANESCO na sasa, “Dispute” haipo, na hivyo Serikali yeyote makini haina sababu ya kuzuia fedha ambazo zipo kwenye akaunti ya Escrow kwa sababu yoyote ile.


PAP ilivyonunua IPTL
Seth ni msimamizi halali na ana nyaraka za mahakama kuonyesha kuteuliwa kwake kama mwangalizi mkuu wa mali zote za Mechmar hapa nchini,lakini b
aadaye Sethi alinunua hisa zote ambazo awali Mechmar alikuwa ameuza kwa Piperlink na kuzihamishia PAP.na hivyo akawa mmiliki wa 70% za hisa za iptl.Sethi baadaye alinunua asilimia 30 zilizosalia, na tayari mmiliki wa VIP, Rugemalira amekwishakiri kupokea Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni) alizoziita kuwa ni fedha za ugoro.baada ya mauzo hayo, VIP ilikwenda mahakamani na kuomba kesi zote zinazohusu kampuni hiyo na Mechmar zifutwe.Septemba 5, mwaka jana, mahakama iliamua kufuta kesi hizo, hivyo PAP akapata haki ya kumiliki mali zote za IPTL, ikiwa ni pamoja na fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow.PAP ilikubali kulipa madeni yote ya IPTL na ufilisi wa muda uliokuwa umewekwa kwa kampuni hiyo uliondolewa.
Kutokana na hukumu ya Mhe. Jaji Utamwa ya tarehe 05 Septemba, 2013 kuondoa IPTL kwenye ufilisi na kutambua PAP kama mmiliki kwa asilimia 100 wa IPTL, TANESCO ilifanya mazungumzo na IPTL kwa ajili usuluhisho wa hesabu ya fedha ambazo TANESCO ilikuwa haijaweka kwenye Akaunti ya Escrow na kukubaliana jinsi ya kulipa fedha hizo.

NINI KIPO NYUMA YA SAKATA HILI LA IPTL

wanajamvi sakata la IPTL ni kiini macho kilichotengenezwa na baadhi ya wanasiasa walioaminiwa na umma ili kuwachafua wanasiasa wenzao wenye heshima mbele ya watanzania kwa minajiri ya kujijenga kisisasa tunapoelekea uchaguzi mkuu mwakani.

CAG
Huyu amekubali kuweka kapuni weredi wake na kukubali kutumika na wanasiasa wanaotafuta umaarufu kama kafulila ambaye anafanya nae kazi kwa karibu kiasi cha kumvujishia ripoti anayopanga kuiwasilisha bungeni kabla hata hajawasilisha, imefikia mahali kafulila amekuwa kama msemaji wa CAG,mpaka kutangazia watu siku ya kustaafu CAG,na chanzo cha ndani kinatueleza bilaa kumung'unya maneno kwamba kabla ya CAG hajastaafu hivi karibuni atahakikisha anang'oka na watu ambao wengine wana matarajio makubwa ya kisiasa na wanaaminiwa na umma wa watanzania kwa kiasi kikubwa,lakini kubwa zaidi ripoti hiyo imedokeza kuwa inakwenda mwiba kwa wawekezaji wa kigeni.

REGINALD MENGI
Huyu ni mmoja wa watu ambao mpaka sasa chanzo kimedokeza ana ripoti hiyo ya CAG kabla haijafikia mamlaka za serikali, Mengi ni mmoja wa wafanyabiashara walio nyuma ya sakata hili la IPTL kwa kujivika uzawa ili kujenga chuki dhidi ya wawekezaji wa kigeni waliowekeza hasa katika sekta ya nishati na madini,na ana ugomvi binafsi na waziri wa nishati na madini,prof sospeter muhongo kwa kusimamia haki na usawa katika uwekezaji bila ubaguzi,Mengi amesikika mara kadhaa akisema atamkomoa Muhongo.

list hii ya watu hawa waliojificha nyuma ya kivuli cha IPTL ili kuchafua wengine itaendelea...

No comments:

Post a Comment