KUTOKA JAMIIFORUMS.
Kufuatia minong’ono ya Hapa na Pale kwamba ndugu EDWARD LOWASSA kuwa
amedhamiria kwenda IKULU hata kwa KUKIPASUA CHAMA chake,
Kwa Mtazamo wangu na wa watu walio wengi, Hizi Hapa CHANGAMOTO KUU
zinazomkabili LOWASSA kutimiza ndoto yake hiyo.
1.
UFISADI
Popote linapotajwa jina la EDWARD LOWASSA, Idea ya kwanza inayokuja
kichwani kwa msikilizaji ni UFISADI ULIOTUKUKA, kwamba kila Watanzania wanapoikumbuka RICHMOND, wanamkumbuka
LOWASSA, kwamba kila leo LOWASSA analipwa na Serikali MABILIONI YA PESA kupitia
UFISADI WA RICHMOND.
Ni vigumu sana kumtenganisha LOWASSA na RICHMOND, LOWASSA ni RICHMOND na
RICHMOND ndo LOWASSA, hili halikwepeki, na Watanzania sio wepesi wa Kusahau
kiasi hicho,
Upo UFISADI mwingi uliofanywa na LOWASSA, katika wizara zote alizowahi kuzitumikia
na nafasi zote alizowahi kuongoza, kwa sasa itoshe tu kusema LOWASSA ni
KIELELEZO KIKUU CHA UFISADI WA TAIFA HILI.
2.
UTAJIRI
MKUBWA
Yawezekana ni Kutokana na UFISADI
wake anaoufanya, lakini ukweli ni Kwamba LOWASSA ni tajiri ambaye hata hawezi kusema
mali zak amezipataje pataje, pamoja na kumiliki mali nyingi hapa Tanzania,
nyingi kati ya hizo akitumia majina ya watoto zake na Maswahiba zake, lakini
LOWASSA ni Miongoni mwa Watanzania wanaomiliki Mali nje ya Nchi,
Unaweza Ukajiuliza Mtumishi huyu
wa Serikali wa miaka mingi aliwezaje Kumiliki NYUMBA TATU za kifahari NCHINI
UINGEREZA?, NYUMBA ZA MABILLIONI YA SHILINGI, alitoa wapi utajiri huo?.
Gazti la RAIA MWEMA NOV.2010
lilitoa MOJA KATI YA PICHA YA MAJUMBA YA LOWASSA NCHINI UINGERZA.
Leo anazunguka kugawa pesa hizi
chafu makanisani na misikitini, UTAJIRI HUU UNA MASHAKA MAKUBWA.
3.
AFYA
MGOGORO.
Kama kuna jambo linawatesa wapambe wa LOWASSA
ni kudorora kwa AFYA yake kila kukicha,
Sio siri tena kwamba LOWASSA ni mgonjwa,
Pamoja na jitihada zinazofanywa na wapamb
wake, kumpeleka UJERUMANI kila MWEZI kupata matibabu, Kumpatia WAGANGA wa
KIENYEJI, kumpeleka mpaka kwa NABII JOSHUA ili aombewe, lakini Hali ya AFYA ya
LOWASSA inazidi kuwa MBOVU kila kukicha.
Sasa hivi hawezi hata kushika kikombe kwa
dakika 5 mfululizo, amedhoofika mno
Juzi alikwenda KARAGWE kumtembelea BALOZI RUHINDA ambaye amepata STROKE
upande mmoja wa mwili wake,
Cha kushangaza BALOZI RUHINDA ameonekana yupo
STRONG MARA DUFU kulinganisha na aliyekuja kumuona, Lowassa ameshindwa hata
kutembea na mgonjwa, matokeo yak akaanguka zaidi ya mara tatu kwenye ngazi.
Jioni yake akashindwa hata kwenda kwenye
Warsha aliyoandasliwa. Hii ni Hatari
Hata wapambe wake alioongozana nao ambao ni
NAZIR KARAMAGI na MUSHI ambaye ni katibu wa CCM MKOA KAGERA walionyesha
kufedheheka kwa namna hali ilivyokuwa.
Sasa hivi LOWASSA ameonekana kupoteza
matumaini ya kugombea tena URAIS, wapambe wake hawana matumaini na Afya yake nay
eye mwenyewe hana tena matumaini.
Kwa Afya ya LOWASSA hakuna muujiza utakaomuwezesha
kumudu na kuhimili heka heka za kampeni za kufanya mikutano zaidi ya 10 kwa
siku.
4.
KUKATALIWA
NA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE
Kila mmoja anaijua nafasi ya mwalimu nyerere
kwenye maisha ya siasa za Tanzania.
Mwalimu Tangu zamani alionyesha kutokumkubali
kabisa LOWASSA, na kwamba UTAJIRI WAKE, UBINAFSI WAKE, UFISADI wake na dhuruma
zake nyingi alizozifanya zilimpelekea mwalimu kuwa hataki hata kumsikia
akishika nafasi kubwa za uongozi kwenye Taifa letu.
LOWASSA, ndio mgombea pekee anayepigiwa UPATU
na viongozi na wanachama wa CHADEMA na vyama vingine vya UPINZANI, sababu kuu
ya kumpigia UPATU huo ni kwamba, wanaamini kuwa LOWASSA ndio mgombea pekee
ambaye ni Dhaifu na mwenye Kashfa na UBADHILIFU mkubwa kwa Taifa hili hivyo
kuwarahishia njia ya kumuangusha na wao kushinda dola. Ndio maana huwezi
kusikia popote Dkt.Slaa ama MBOWE akimsema vibaya LOWASSA.
No comments:
Post a Comment