KARIBU SANA
Friday, 11 July 2014
JANUARY MAKAMBA SASA AFUNGUKA TENA
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia,January Makamba amesema Taifa linahitaji maarifa mapya ya kuisukuma nchi kimaendeleo.
Amesema anaamini yeye ni miongoni mwa watu wenye nafasi ya kutoa mchango wake katika kufanikisha hilo.
Pia amesemaq kuna haja ya kuwepo kwa utaratibu kwa wanaoomba nafasi za uongozi wa ngazi mbalimbali,hasa za juu nchini,kujitangaza mapema ili kutoa fursa ya kujadiliwa na kupimwa na watanzania
Amesema hatua hiyo itasaidia kuanzisha mijadala kuhusu sifa za viongozi na wanaohitajika kulingana na mahitaji pamoja na kuangalia uwezo na maarifa ya wahusika.
Alisema hayo jana alipozungumza na Uhuru kuhusu yaliyojitokeza baada ya kutangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwakani,ambapo alisema ni vyema kuwe na muda wa kutosha wa kuwajua wagombea ili watu wasishtukizwe dakika ya mwisho...Source Gazeti la Uhuru
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment