Ampongeza kwa uwezo wake
amsifia kwa uwajibikaji wake
amtakia kila la heri kwenye safari yake. hii hapa sehemu ya maneno ya JK kama yalivyonaswa kutokea BUMBULI
Alichokisema
Rais ni hiki
Kauli ya JK kama ilivyonaswa akiwa Bumbuli:
''January anafanya kazi nzuri
ya Ubunge. Pia ananisaidia sana kwa kazi ya Wizara niliyompa. Unajua
January alipogombea Ubunge alinificha. Nilikuwa nasikia kwa wenzake tu
pale ofisini.
Baadaye alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia
kwamba Mzee na Mimi najitosa. Nikamtakia heri. Kwa kweli kwa jinsi
anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka Kwa dhati kabisa
ya kusaidia watu wa Bumbuli. Nimesikia anafikiria mambo makubwa.
Hajaniambia. Mi Nimesikia tu. Namtakia kila la heri.
Haya mambo anaamua
Mungu. Wala hayalazimishwi. Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote
hawataki. Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi
haliwezi kuwa. Mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika
wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani. Kama halijafika
wakati wake haliwezi kutokea.
Mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu
haikuwa wakati wake. 2005 ikawa wakati wake nikapata. Na wewe usipopata
sasa usiweke nongwa"
No comments:
Post a Comment