KARIBU SANA

Wednesday, 18 June 2014

UHISPANIA YAAGA KOMBE LA DUNIA BRAZIL


Kufuatia ushindi huu wa mabao 2-0 mikononi mwa Chile mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania sasa wamehakiki tikiti za ndege kurejea nyumbani pamoja na Australia .
Hii ni baada ya Uholanzi kushinda mechi yake ya pili na kuongoza kundi B ikiwa na alama 6 sawa na Chile.
Chile na Uholanzi hata hivyo zitakutana katika mechi ya kuamua yupi kati yao ataongoza kundi hilo.
Mshindi wa pili katika kundi B atachuana na bingwa katika kundi A inayojumuisha wenyeji Brazil na washindi wa pili katika kundi hilo Mexico.
Kwa upande wao Uhispania ambao sasa wamefungwa jumla ya mabao 7 watachuana na Australia katika mechi ambayo haitakuwa na umuhimu wowote .
23:54 Mechi imekamilika Uhispania 0-2 Chile
23:49 Dakika 6 za ziada zitachezwa kuamua iwapo Uhispania wataiacha kombe la dunia Brazil na kurejea nyumbani mapema

Uhispania wanakodolea jicho safari ya kurudi nyumbani 

23:49 Uhispania 0-2 Chile
23:48 Dakika 3 za mwisho matokeo bado ni yaleyale ya kipindi cha kwanza
23:47 Bravo anaudaka bila wasiwasi
23:47 Freekick Kuelekea lango la Chile.
23:43 Iniesta anamlazimu Bravo kuutema nje mkwaju wake na ni Kona kuelekea Chile
23:42 Australia na Uhispania hawajashinda mechi yeyote Brazil 2014
23:41Kufuatia matokeo ya mechi iliyotangulia Uholanzi inaongoza kundi B ikiwa na alama 6 huku Chile ikiwa na alama sawa na hizo
23:40 Uhispania inachini ya dakika 10 sasa kufunga mabao mawili amawajipange kuabiri ndege ya kurejea nyumbani
23:30 Mwaka wa 2010 Italia walitua Afrika Kusini lakini wakashindwa katika hatua ya makundi
23:29 Mabingwa wa tiki taka wanafunzwa mfumo mpya wa soka na Chile
23:26 Andrés Iniesta anakosa kuitumia ipasavyo nafasi hiyo


Huzuni miongoni mwa mashabiki wa Uhispania 

23:26 Freekick Francisco Silva (Chile).
23:23 Fernando Torres anaingia , Diego Costa anapumzishwa
23:19 Fernando Torres anajianda kuingia kocha Del Bosque akitafuta uokozi katika mechi hii zikiwa zimesalia dakika 30 pekee ya mechi hii
23:16 Uhispania 0-2 Chile 56''
23:15 Uhispania wanakodolea jicho safari ya kurudi nyumbaniiwapo mechi hii itamalizika hivi ilivyo
23:12 Sergio Ramos anapoteza nafasi ya kuinusuru dau lao anapopiga nje mpira
23:12 Freekick kuelekea lango la Chile
23:11 Koke anaangushwa mbele ya lango
23:10 Mauricio Isla anaupoteza mpira huku Uhispania ikifanya mashambulizi.
23:08 Diego Costa anakosa nafasi mbele ya lango la Chile inakuwa Kona lakini inazuiliwa na safu ya ulinzi ya Chile
23:04 Kipindi cha pili kinaanza katika mechi hii ya kihistoria kati ya Chile na Mabingwa watetezi Uhispania
23:03 Koke anajiandaa kuingia katika ile nafasi iliyokuwa imechukuliwa na Xavi Alonso
22:45 Hii ndiyo itayokuwa mara ya kwanza kwa bingwa mtetezi kushindwa katika mechi mbili za kwanza za kombe la dunia .

Vargas akishangilia kuilaza Uhispania 

22:45 Iwapo mechi hii itakamilika ilivyo sasa ,Uhispania watakuwa hawana budi ila kuelekea nyumbani
22:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika.
22;44 UHISPANIA 0-2 CHILE
22:44 Uhispania inafungwa bao la pili kutokana na mkwaju wa Charles Aranguiz
22:43 GOOOOOOOAL
22:42FREEKICK kuelekea upande wa Uhispania unatemwa na Cassilas
22:42 Mechi hii inachezewa katika nusu ya Uhispania huku chile ikiendeleza mashambulizi
22:40 Xavi Alonso anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea visivyo Isla
22:31 Iniesta anaupoteza mpira na sasa ni Freekick kwa upande wa Chile ambayo inachukuliwa kwa haraka .
22:30 Freekick kuelekea kwa lango la Chile
22:28 Refarii Mark Geiger anatoa kadi yake ya kwanza ya njano katika mechi hii kwa Vidal
22:27 Chile wanaanza nipe nikupe kati ya Sanchez na Mena
22:26 Diego Costa anafyatua mkwaju unaogonge upande wa nje wa neti
22:26 Kipa wa Uhispania Iker Cassillas awazomea walinzi wake kwa kuruhusu mashambulizi .

Kocha wa Uhispania Del Bosque

22:20 Eduardo Vargaz aipatia Chile bao muhimu dhidi ya mabingwa watetezi
22:19 Chile wanapata bao lao la kwanza kupitia kwa Vargaz dakika ya 19
22:19 GOOOOOOOAL
22:18 Chile inaendelea na mashambulizi kuelekea a Uhispania Bado mechi hii haijatulia
22:16 Goalkick kuelekea lango la Uhispania
22:14 Alonso anapoteza nafasi ambayo ni ya ana kwa ana na kipa wa Chile Bravo
22:13 Alonso anaupoteza mpira na kuonekana kumkera Del Bosque
22:13 Freekick Kuelekea lango la Chile inayopigwa na Alonso.
22:04 Kiti cha Kocha wa Uhispania Del Bosque kimekuwa moto tayari
22:03 Iker Cassillas anajikakamua na kuudaka bila wasiwasi.
22:02 KONA. kuelekea upande wa Uhispania
22:02 Mpira umeanza na Chile wanafanya shambulizi la mapema ambalo Alonso na Uhispania hawana jibu inakuwa ni Kona.

Uhispania ililazwa 5-1 na Uholanzi katika mechi yao ya kwanza 

21:55 wimbo wa taifa wa uhispania unachezwa sasa .
21:50 Timu zinaingia uwanjani sasa
21:48 Australia imefungwa mabao matatu huku Uhispania ikiwa imefungwa mabao manne.
21:48 Chile ni ya pili ikiwa na alama tatu huku Australia licha ya kushindwa katika mechi mbili ikiwa ya tatu kutokana na uchache wa mabao.
21:48 Uholanzi inaongoza kundi B ikiwa na jumla ya alama 6.
21:47 Australia imeshindwa katika mechi ya pili dhidi ya Uholanzi mabao 3-2
21:46 Timu ya Chile ilishinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Australia 3-1

Uhispania inatufuta ushindi wa kwanza katika kombe la dunia Brazil.

21:45 Uhispania ililazwa mabao 5-1 na Uholanzi katika mechi yao ya ufunguzi.
21:45 Mabingwa watetezi Uhispania wanatafuta ushindi dhidi ya Chile baada ya kushindwa na Uholanzi katika mechi yao ya kwanza ya kombe la dunia Brazil.

BBC.

No comments:

Post a Comment