Uingereza imesisitiza kuwa marufuku iliyowekewa mmea
wa Miraa itaanza kutekelezwa tarehe 24 mwezi Juni. Hii inafuatia bunge
la nchi hiyo kupitisha uamuzi wa serikali ya Uingereza kuorodhesha miraa
katika kundi la dawa za kulevya.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Uingereza
imesema kuwa uamuzi huo haulengi Kenya moja kwa moja. Imeongeza kuwa
Serikali ya Uingereza imekuwa ikidhamiria kwa muda mrefu kuchunguza
kisheria hali ya mmea huo.Wabunge hao walikuwa wamesema kuwa wakulima wa mmea huo watapata hasara kubwa kwa sababu walikuwa wakiutegemea kukuza uchumi wa eneo hilo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Uingereza ilichukua uamuzi huo baada ya kushauriana na washiriki wake.
Nchi nyingi zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi yaani G8 zikiwemo Canada na Marekani zimeharamisha Miraa iliyotajwa kuwa miongoni mwa dawa za kulevya.
Mswada wa kupiga marufuku mmea huo unaotumia mno Uingereza ulijadiliwa bungeni machi na kuidhinishwa na bunge la chini na lile la juu baadaye hivyo kuwa sheria.
No comments:
Post a Comment