KARIBU SANA

Wednesday, 18 June 2014

MEMBE AMKANA MASELE. AMSAFISHA BALOZI WA UINGEREZA


Taarifa zimesambaa kuwa Usiku wa tarehe 18.06.2014 waziri wa mambo ya Nje Bernad Membe akiwa nyumbani kwa balozi wa UK Diane Melrose. Kwenye hafla ya siku ya kuzaliwa ya Malkia Elizabeth amesisitiza mbele ya mabalozi wa mataifa mbalimbali kuwa tuhuma alizotoa masele dhidi ya Uingereza na balozi wakati akijitahidi kupangua tuhuma za escrow serikali imejiridhisha kuwa hazina ukweli wowote kadili ya ushahidi uliowasilishwa na masele serikalini

Membe also said that the PM will issue a public statement tomorrow to announce that the BHC has been cleared of all allegations.

WALIPUAJI WA BOMU WAKAMATWA

Washukiwa wa mauaji Mpeketoni wakamatwa

Uharibifu na mauaji yaliyoshuhudiwa Mpeketoni yamefananishwa na hali iliyotokea Westgate mwaka jana

Polisi nchini Kenya wamesema kuwa wamewakamata washukiwa wawili wa mashambulizi yaliyofanyika mjini Mpeketoni, Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60.
Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab limekiri kufanya mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumapili usiki na Jumatatu usiku ingawa serikali ya Kenya imesema kuwa mashambulizi hayo yalichochewa kisiasa.
''Tumewakamata watu kadhaa kuhusiana na mashambulizi ya Mpeketoni, akiwemo miliki wa gari moja lililotumika katika mashambulizi hayo,'' alinukuliwa akisema mkuu wa polisi David Kimaiyo.
Wakazi wa Mpeketoni wakiwa na huzuni kutokana na yaliyowakumba 

Mshukiwa wa pili aliyekuwa anaandika kwenye akaunti ya Twitter inayoshukiwa kumilikiwa na Al Shabaab pia alikamatwa. Anadaiwa kutangaza kuwa Al Shabaab ndio waliofanya mashambulizi hayo
Licha ya madai ya haraka kutoka kwa kundi la Al Shabaab kuwa wao ndio waliotekeleza mashmabulizi hayo, Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa taifa alilaumu vikundi vya wanasiasa pamoja na makundi ya watu ambayo yana nia ya kufaidi kutokana na hali mbaya ya usalama nchini humo kwa kufanya mashambulizi hayo.
Maafisa kadhaa wa polisi wa eneo la Mpeketoni, wamefutwa kazi na wengine kuhamishwa kutoka vituo vyao vya kazi katika eneo hilo.
Hii ni baada ya tuhuma dhidi yao kuwa walipuuza onyo la kutokea kwa mashambulizi hayo kutoka kwa shirika la ujasusi. Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

BBC

IRAQ YAOMBA MSAADA MAREKANI

Njooni mtusaidie - Iraq kwa Marekani

Majeshi ya angani ya MArekani kutumwa Iraq

Iraq imeomba rasmi usaidizi wa Marekani kushambulia kwa ndege wapiganaji wa kiislamu walioteka miji kadhaa nchini humo wiki hii.
"Tumepokea ombi kutoka kwa serikali ya Iraq kutumia ndege zetu huko,'' alithibitisha kamanda mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Martin Dempsey mbele ya baraza la senate.

ISIS waendeleza harakati zao

wapiganaji wa ISIS wameilemea serikali ya Iraq

Awali wapiganaji hao wa madhehebu ya Sunni walishambulia kiwanda kikubwa zaidi cha kusafishia mafuta nchini Iraq katika mji wa Baiji kaskazini mwa Baghdad.
Katika taarifa yake kwa taifa, waziri mkuu Nouri AL Maliki alitoa wito kwa raia wa Iraq waungane dhidi ya wanamgambo.
Vikosi vya jeshi vinajitahidi kuwakabili na kuwasukuma nje wanamgambo wa ISIS pamoja na washirika wao wa Ki-sunni kutoka mikoa ya Diyala na Salahuddin baada ya waasi hao kuteka mji wa Mosul wiki iliyopita.

Obama ataka kuisaidia Iraq

Na hapo Jumatano, rais Barack Obama alifanya kikao cha dharura na baraza la Congress kujadili mzozo wa Iraq.
Duru za ikulu ya White house zinasema kuwa Bwana Obama ''amependekeza kuongezwa juhudi zetu nchini Iraq na kusaidia majeshi ya serikali hiyo katika kukabiliana na wanamgambo wa ISIS ikiwemo uwezekano wa kuongeza usaidizi wa kiusalama''.

Baadhi wanapinga

Lakini kabla ya kufanyika mkutano huo, kinara wa baraza la Senatae wa Marekani Harry Reid, kutoka chama cha Demokrats alisema kuwa hakubaliani kamwe na wazo la kuihusisha Marekani katika ''vita vya ndani vya Iraq''.
Marekani imekuwa katika ubishi mkubwa katika mabunge ya Senate na Congress juu ya kuondolewa majeshi yao ndani ya Iraq na Afghanistan

BBC

CAMEROON YAFUNGASHA VIRAGO BRAZIL


02:33 Cameroon bila shaka sasa wanakuwa timu ya tatu kuelekea nyumbani na ya kwanza kutoka Afrika kufunganya virago.
02:31 Croatia 4-0 Cameroon
02:31 Mandzukic anafunga bao la nne la Croatia
02:31 Croatia 4-0 Cameroon 73''
02:19 Croatia 3-0 Cameroon
02:18 Mandzukic anafunga bao la tatu la Croatia
02:18 GOOOOAL
02:17 Itandje anakunguwaa lakini mpira unatoka nje na inakuwa KONA kuelekea Cameroon
02:16 Croatia 2-0 Cameroon
02:15 Srna anaupiga nje
02:13 FREEKICK kuelekea upande wa Cameroon nje ya eneo
02:12 Kipa wa Cameroon Itandje atajilaumu kwa bao hilo la pili ambalo hakuwa makini
02:11 Cameroon bila shaka sasa wanakuwa timu ya tatu kuelekea nyumbani na ya kwanza kutoka Afrika
02:09 Mandzukic amesalia peke yake na kipa wa Cameroon lakini anaupiga mpira nje ,,,,
02:09 croatia wanashambulia tena
02:09 Croatia 2-0 Cameroon
02:08 Peresic anaiweka Croatia mbele kwa bao la pili
02:08 GOOOAL
02:07 Croatia wanafanya mashambulizi
02:04 Kipindi cha pili kimeanza Cameroon 0-1 Croatia
01:45 Matumaini ya Cameroon kufuzu kwa raundi ya pili sasa yamepata pigo kubwa na itawalazimu kujifunga kibwebwe angalau kusaawazisha katika dakika 45 zzilizosalia.
01:45 Alexandre Song ametimuliwa uwanjani baada ya kumkomoa Mandzukic mgongoni na sasa Cameroon wamesalia wachezaji 10 uwanjani .
01:45 Cameroon 0-1 Croatia
01:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika .
01:44 Shambulizi la Cameroon likiongozwa na Aboubakar linakomeshwa
01:41 Cameroon sasa wanalazimika kucheza salio la mechi hii wakiwa watu kumi uwanjani.


Cameroon 0-1 Croatia 

01:40 Song anaonekana kumgonga Mandzukic kutoka nyuma na refarii mreno Pedro Proenca
01:39 Alexander Song anaoneshwa kadi Nyekundu
01:36 Fastbreak kuelekea upande wa Cameroon lakini Song anaumega mpira na kugeuza na kuwa shambulizi kuelekea lango la Croatia akisaidiana na Mbia
01:34 Mandzukic anaongoza mashambulizi ambayo kipa Itandje anautema nje na inakuwa ni Kona.
01:33 Mbia anakuwa mchoyo na mpira na anaupoteza katika eneo la lango la Croatia
01:26 Iwapo Cameroon wataendelea kupena mpira hivi huenda wakawa timu ya tatu kuyaaga mashindano haya ya kombe la Dunia
01:25 Cameroon 0-1 Croatia
01:23 Stephanie Mbia anapoteza umiliki lakini Matip anapeana Freekick
01:22 KONA kuelekea Croatia
01:20 Mbia anapoteza nafasi nzuri ya kusawazishia Cameroon anaupiga mpira nje .
01:19 Luka Modric anaangushwa nje ya eneo na Matip
01:18 Mandzukic anaongosha mashambulizi katika lango la Cameroon
01:14 Croatia wanatawala mechi hii katika dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza
01:12 Croatia 1-0 Cameroon
01:11 Croatia wanapata bao la kwanza kupitia kwa Olic
01:10 BAOOOOOOOO

Timu ya Cameroon 

01:09 Mario Mandzukic anamchenga Chedou
01:05 Mbia anaonywa na refarii Pedro Proenca
01:04 Vincent Aboubakar (Cameroon) anaangushwa na Cameroon inapewa freekick

Mashabiki wa Croatia 

01:02 Cameroon inapata Freekick ya kwanza inayopigwa na A. Song
01:00 Mechi imeanza katika uwanja wa Amazonia ulioko Manus

Timu ya Croatia 

00:59Timu mbili za kwanza katika kila kundi ndizo zinazosonga mbele
00:58 Timu zote kwa hivyo zitajitahidi kushinda mechi hii angalu kuokoa ari yao ya kufuzu kwa mkondo wa pili.

Etoo hatocheza dhidi ya Croatia 

00:57Cameroon itakuwa bila ya nyota wake Samuel Etoo ambaye anauguza jeraha la goti
00:56 Cameroon kwa upande wake ilipoteza 1-0 dhidi ya Mexico katika mechi yao ya kwanza .
00:56 Croatia ilizimwa 3-1 na Brazil katika mechi ya ufunguzi
00:56 Croatia inachuana na Cameroon kwa mara ya kwanza katika fainali za kombe la dunia .
BBC.

UHISPANIA YAAGA KOMBE LA DUNIA BRAZIL


Kufuatia ushindi huu wa mabao 2-0 mikononi mwa Chile mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania sasa wamehakiki tikiti za ndege kurejea nyumbani pamoja na Australia .
Hii ni baada ya Uholanzi kushinda mechi yake ya pili na kuongoza kundi B ikiwa na alama 6 sawa na Chile.
Chile na Uholanzi hata hivyo zitakutana katika mechi ya kuamua yupi kati yao ataongoza kundi hilo.
Mshindi wa pili katika kundi B atachuana na bingwa katika kundi A inayojumuisha wenyeji Brazil na washindi wa pili katika kundi hilo Mexico.
Kwa upande wao Uhispania ambao sasa wamefungwa jumla ya mabao 7 watachuana na Australia katika mechi ambayo haitakuwa na umuhimu wowote .
23:54 Mechi imekamilika Uhispania 0-2 Chile
23:49 Dakika 6 za ziada zitachezwa kuamua iwapo Uhispania wataiacha kombe la dunia Brazil na kurejea nyumbani mapema

Uhispania wanakodolea jicho safari ya kurudi nyumbani 

23:49 Uhispania 0-2 Chile
23:48 Dakika 3 za mwisho matokeo bado ni yaleyale ya kipindi cha kwanza
23:47 Bravo anaudaka bila wasiwasi
23:47 Freekick Kuelekea lango la Chile.
23:43 Iniesta anamlazimu Bravo kuutema nje mkwaju wake na ni Kona kuelekea Chile
23:42 Australia na Uhispania hawajashinda mechi yeyote Brazil 2014
23:41Kufuatia matokeo ya mechi iliyotangulia Uholanzi inaongoza kundi B ikiwa na alama 6 huku Chile ikiwa na alama sawa na hizo
23:40 Uhispania inachini ya dakika 10 sasa kufunga mabao mawili amawajipange kuabiri ndege ya kurejea nyumbani
23:30 Mwaka wa 2010 Italia walitua Afrika Kusini lakini wakashindwa katika hatua ya makundi
23:29 Mabingwa wa tiki taka wanafunzwa mfumo mpya wa soka na Chile
23:26 Andrés Iniesta anakosa kuitumia ipasavyo nafasi hiyo


Huzuni miongoni mwa mashabiki wa Uhispania 

23:26 Freekick Francisco Silva (Chile).
23:23 Fernando Torres anaingia , Diego Costa anapumzishwa
23:19 Fernando Torres anajianda kuingia kocha Del Bosque akitafuta uokozi katika mechi hii zikiwa zimesalia dakika 30 pekee ya mechi hii
23:16 Uhispania 0-2 Chile 56''
23:15 Uhispania wanakodolea jicho safari ya kurudi nyumbaniiwapo mechi hii itamalizika hivi ilivyo
23:12 Sergio Ramos anapoteza nafasi ya kuinusuru dau lao anapopiga nje mpira
23:12 Freekick kuelekea lango la Chile
23:11 Koke anaangushwa mbele ya lango
23:10 Mauricio Isla anaupoteza mpira huku Uhispania ikifanya mashambulizi.
23:08 Diego Costa anakosa nafasi mbele ya lango la Chile inakuwa Kona lakini inazuiliwa na safu ya ulinzi ya Chile
23:04 Kipindi cha pili kinaanza katika mechi hii ya kihistoria kati ya Chile na Mabingwa watetezi Uhispania
23:03 Koke anajiandaa kuingia katika ile nafasi iliyokuwa imechukuliwa na Xavi Alonso
22:45 Hii ndiyo itayokuwa mara ya kwanza kwa bingwa mtetezi kushindwa katika mechi mbili za kwanza za kombe la dunia .

Vargas akishangilia kuilaza Uhispania 

22:45 Iwapo mechi hii itakamilika ilivyo sasa ,Uhispania watakuwa hawana budi ila kuelekea nyumbani
22:45 Kipindi cha kwanza kimekamilika.
22;44 UHISPANIA 0-2 CHILE
22:44 Uhispania inafungwa bao la pili kutokana na mkwaju wa Charles Aranguiz
22:43 GOOOOOOOAL
22:42FREEKICK kuelekea upande wa Uhispania unatemwa na Cassilas
22:42 Mechi hii inachezewa katika nusu ya Uhispania huku chile ikiendeleza mashambulizi
22:40 Xavi Alonso anaoneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea visivyo Isla
22:31 Iniesta anaupoteza mpira na sasa ni Freekick kwa upande wa Chile ambayo inachukuliwa kwa haraka .
22:30 Freekick kuelekea kwa lango la Chile
22:28 Refarii Mark Geiger anatoa kadi yake ya kwanza ya njano katika mechi hii kwa Vidal
22:27 Chile wanaanza nipe nikupe kati ya Sanchez na Mena
22:26 Diego Costa anafyatua mkwaju unaogonge upande wa nje wa neti
22:26 Kipa wa Uhispania Iker Cassillas awazomea walinzi wake kwa kuruhusu mashambulizi .

Kocha wa Uhispania Del Bosque

22:20 Eduardo Vargaz aipatia Chile bao muhimu dhidi ya mabingwa watetezi
22:19 Chile wanapata bao lao la kwanza kupitia kwa Vargaz dakika ya 19
22:19 GOOOOOOOAL
22:18 Chile inaendelea na mashambulizi kuelekea a Uhispania Bado mechi hii haijatulia
22:16 Goalkick kuelekea lango la Uhispania
22:14 Alonso anapoteza nafasi ambayo ni ya ana kwa ana na kipa wa Chile Bravo
22:13 Alonso anaupoteza mpira na kuonekana kumkera Del Bosque
22:13 Freekick Kuelekea lango la Chile inayopigwa na Alonso.
22:04 Kiti cha Kocha wa Uhispania Del Bosque kimekuwa moto tayari
22:03 Iker Cassillas anajikakamua na kuudaka bila wasiwasi.
22:02 KONA. kuelekea upande wa Uhispania
22:02 Mpira umeanza na Chile wanafanya shambulizi la mapema ambalo Alonso na Uhispania hawana jibu inakuwa ni Kona.

Uhispania ililazwa 5-1 na Uholanzi katika mechi yao ya kwanza 

21:55 wimbo wa taifa wa uhispania unachezwa sasa .
21:50 Timu zinaingia uwanjani sasa
21:48 Australia imefungwa mabao matatu huku Uhispania ikiwa imefungwa mabao manne.
21:48 Chile ni ya pili ikiwa na alama tatu huku Australia licha ya kushindwa katika mechi mbili ikiwa ya tatu kutokana na uchache wa mabao.
21:48 Uholanzi inaongoza kundi B ikiwa na jumla ya alama 6.
21:47 Australia imeshindwa katika mechi ya pili dhidi ya Uholanzi mabao 3-2
21:46 Timu ya Chile ilishinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Australia 3-1

Uhispania inatufuta ushindi wa kwanza katika kombe la dunia Brazil.

21:45 Uhispania ililazwa mabao 5-1 na Uholanzi katika mechi yao ya ufunguzi.
21:45 Mabingwa watetezi Uhispania wanatafuta ushindi dhidi ya Chile baada ya kushindwa na Uholanzi katika mechi yao ya kwanza ya kombe la dunia Brazil.

BBC.

CAMEROON YACHAPWA 4-0

Alexander Song itabidi ajilaumu kwa kujisaabishia kadi nyekundu ya kizembe baada ya kumpiga ngumi ya makusudi kiungo wa croatia.

kutolewa nje kwa Song kumeisababisha Cameroon kucheza chini ya kiwango na kuruhusu kufungwa magoli 4 matatu yakipatikana kipindi cha pili.
kwa matokeo hayo sasa Cameroon inaungana na Hispania kwenye safari ya kurudi nyumbani baada ya Hispania kuaga mashindano mapema kwa kukubali kulala mabao 2 bila majibu dhidi ya Chile.

Thursday, 12 June 2014

HUYU NDIYE KASA ALIYEITABIRIA BRAZIL KUIFUNGA CROATIA LEO #BRAZUKA


BAADA ya pweza Paul aliyekuwa akiishi Ujerumani kujizolea umaarufu wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, fainali za mwaka huu nchini Brazil ameibuka mtabiri mwingine aitwaye Cabeção au Big Head.

Big Head ambaye ni kasa mwenye umri wa miaka 25, anayeishi katika kijiji cha Praia Do Forte nchini Brazil ameitabiria nchi yake ya Brazil kuibuka na ushindi katika mechi ya ufunguzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Croatia kesho.

Big Head ameanza kazi yake hiyo jana, Jumanne kwa kutabiri mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia. Kasa huyo anafanya utabiri kwa kuchagua vyakula. Alichagua mmoja wa samaki waliokuwa wananing'inia katika bendera za Brazil, Croatia na kwenye mpira.

HIVI NDIVYO HALI ILIVYOKUWA SOKONI KARUME


Image00067
Kwa mujibu wa mashuhuda kadhaa waliokuwepo katika eneo la tukio tangu moto huo unatokea, Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ingawa wana wasiwasi na hitilafu ya  umeme iliyojitokeza usiku wa June 10.
Image00047Moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 4 usiku ambapo iliwachukua zaidi ya saa moja kikoasi cha zima moto na uokoaji kufika eneo la tukio. Baadhi ya Wafanyabiashara ambao bidhaa zao zimeteketea kwa moto wamesema kuwa wamepata hasara kubwa ambayo haielezeki kwani baadhi yao wameshindwa kuokoa hata kitu kimoja.
Soko la Karume ni miongoni mwa masoko makubwa ya mitumba yanayotumiwa na wakazi wengi wa jiji la Dar es salaam na maeneo jirani kutokana na urahisi wa bei wa bidhaa zinazopatikana hapo.
Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa asubuhi ya leo baada ya tukio hilo ikionyesha madhara makubwa yaliyotokea baada ya ajali hiyo mbaya.
Image00050
Image00049
Image00046
Image00041
Image00038
Image00037

Image00035
Image00034
Image00033
Image00032
Image00028
Image00024
Image00011
Image00017
Image00020
Image00022
Image00009
Image00008
Image00005
Image00051
Image00063
Image00086
Image00081
Image00079
Image00077
Image00076
Image00066

Image00068
Image00073
Image00074
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

millard.