KARIBU SANA

Monday 22 September 2014

SAKATA LA ESCROW AKAUNTI IPTL YAMKANA PROF. TIBAIJUKA




Mwanasheria IPTL/PAP asema hawhusiki na
fedha za Profesa Tibaijuka

       Joseph Makandege - PAP/IPTL

  Prof. Anna Tibaijuka - Waziri.

SIRI zaidi imezidi kufichuka kuhusiana na sakata la akaunti ya ESCROW na IPTL, ambapo sasa imefahamika malipo yaliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Profesa Anna Tibaijuka alipewa fedha zinazotokana na akaunti hiyo sio kweli, imefahamika.

Pia, inadaiwa fedha hiyo zaidi ya sh. Bilioni 1.6 alizopata Profesa Tibaijuka kutoka kwa mmoja waliokuwa wanahisa wa Kampuni ya kufua umeme ya Independet Power Supply Limited (IPTL), James Rugemalila hazihusiani na akaunti hiyo.

Taarifa zaidi za kuaminika kutoka katika ofisi za IPTL/PAP zilieleza kuwa fedha hizo zilikuwa ni mali ya Rugemalila, ambaye wakati anatoa hizo fedha kwa Tibaijuka hakuwa tena mwanahisa wa IPTL.

Ilisema nyaraka zinaonyesha kwamba, Rugemalila alikwisha uza hisa zake zote alizokuwa anamiliki kupitia kampuni yake ya VIP, ambapo alikuwa anamiliki asilimia 30 na kuziuza kwa Kampuni ya PAP.

Akizungumza kuhusiana na tuhuma hizo, Mwanasheria na Katibu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema katika suala nzima la IPTL ukweli unafichwa na umma hauelezwi.

Alisema tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kueleza ukweli halisi, lakini umekuwa ukipotoshwa kwa maslahi binfasi ya watu.

‘Rugemalila(VIP) aliuza hisa zake zote na kufuata taratibu za kisheria na nyaraka zipo ofisini kwetu na BRELA. Rugemalila hakulipwa fedha za ESCROW, bali alilipwa fedha za kuuza hisa zake,’’alisema.

Makandege aliongeza ‘Mtu mwenye fedha zake kaamua kumpa mtu mwingine ama kwa kumkopesha, kumsaidia au kwa mapenzi yake mwenyewe fedha zake shida iko wapi na IPTL inahusikaje hapa. Nafikiri Rugemalila ndiye anayejua matumizi ya fedha zake,’’.

‘Izingatiwe kwamba fedha za ESCROW sio hisani wala rushwa ni malipo halali yanayotokana na IPTL kuwauzia TANESCO umeme, ambao watanzania wameutumia na wanaendelea kuutumia. Je, wanasiasa walitaka tuwape umeme bure,’’alisema.

Makandege alisema IPTL/PAP ni mmiliki halali aliyefuata taratibu zote na malipo aliopewa kutoka akaunti ya ESCROW ni halali na hakuna vitendo vya ufisadi vyovyote.

‘Umma utakuja kuelewa katika suala hili, wanaozungumza wanatumiwa kwa kuwa IPTL/PAP ndio kampuni inayoiuzia umeme kwa bei nafuu Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kuliko kampuni zote na kinachofanyika ni wivu wa kibiashara,’’alisema.

Hivyo, alisema IPTL/PAP haihusiki na fedha zozote alizopewa Profesa Tibaijuka, ambaye ni Waziri wa Ardhi, Maendeleo na Makazi pamoja na watu wengine wote ikiwa wapo wamepewa na watanzania waepukane na upotoshaji huo.

  

No comments:

Post a Comment