HABIBU MCHANGE AKIJADILI JAMBO
MBOWE AKITETEA JAMBO NA SLAA
TUNDU LISSU
PRESS RELEASE
TAARIFA
YA NDUGU HABIBU MCHANGE KUHUSU KUHUSISHWA NA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WENGINE
ILI KULIPUA HELKOPTA YA SLAA NA MNYIKA ILIYOTOLEWA NA CHADEMA NA MASWALA
MENGINE
TAREHE.14.08.2014.
UTANGULIZI.
Ndugu wanaHabari,
Mtakumbuka kwamba Tarehe
9.08.2014, katika vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya kijamii imeripotiwa Taarifa ya
TUNDU LISSU na waliokuwa MADIWANI wa shinyanga mjini baadae wakahamia CCM,
pamoja na Tuhuma nyingine kwamba
kuliwahi upangwa mpango wa KUILIPUA HELKOPTA iliyowabeba WILBROD SLAA na JOHN MNYIKA ili wafe,
Na wanasema miongoni mwa
waliohusika kufanya mkakati huo ni Ndugu HABIBU MCHANGE, ambaye ni Mimi.
Japo kuwa hii si habari ya
kwanza ya kipuuzi inayotolewa na viongozi wa CHADEMA ikinihusisha mimi ama moja
kwa moja au la, tangu baada ya mgogoro wangu wa kisiasa ndani ya CHADEMA may
2011.
Na habari nyingi kati ya
hizo nimeamua kuzipuuzia, leo ninaomba kusema kidogo ili kuweka kumbukumbu sawa
na sahihi.
KUHUSU
KUILIPUA HELKOPTA.
Pamoja na kwamba hekaya hii
ni ya kipuuzi,
Haingii akilini hata kidogo
kwamba mimi Habibu Mchange Nimepanga na CCM na naibu waziri kuilipua helkopta
ambayo ingewabeba Slaa na Mnyika.
Upuuzi huu ulioratibiwa na
Tundu Lissu, ni uthibitisho wa kushindwa na kuporomoka kisiasa kwa kasi ya ajabu
kunakoikabili CHADEMA kwa sasa, na kujiokoa kwenye hilo wanaanza sasa
kutengeneza tuhuma za kitoto namna hii zisizokuwa na kichwa wala miguu ili
kupata huruma ya wananchi.
Ninawezaje
kupanga mikakati ya kulipua helkopta, ili iwe nini?
Kwangu mimi kwa sasa Slaa ni
miongoni mwa wanansiasa dhaifu waliowahi kutokea kwenye ulimwengu wa siasa za
Tanzania.
Slaa
ameshajiishia, nimlipue ili iwe nini?
Mtu aliyeishiwa ushawishi
kama yeye, kiasi cha kushindwa kumshawishi hata mke wake aliyemzalia watoto
wawili, anawezaje kuwa Tishio na kupangiwa mikakati ya kulipuliwa?
Nasema siwezi kufanya ujinga
wa namna hii na hata kama angekuwa tishio kisiasa, si hurka yangu kujihusisha
na matukio ya KIGAIDI namna hii.
CHADEMA
NA MAUAJI / UJANGILI
SLAA, LISSU, MBOWE, MNYIKA,
LEMA na CHADEMA ndio mabingwa wa matukio ya KIGAIDI na utoaji roho za wenzao,
hasa pale wanapokuwa wametofautiana misimamo na mitazamo ndani ama nje ya
Chama. Tafadhali wasitafute mtu wa kushiriki naye dhambi za mauaji
waliyoyatenda na wanayoendelea kutenda.
Dunia Nzima inajua kwamba
watu hawa wameshiriki kikamilifu kumuondoa DUNIANI aliyekuwa makamu mwenyekiti
wa chama CHACHA ZAKAYO WANGWE, Hii haina ubishi kwamba, MBOWE, SLAA na MNYIKA
walijaribu mara kadhaa kutaka kumuua CHACHA WANGWE kwa kutumia sumu na
kushindwa mpaka walipofanikiwa kumuua kwa ajali ya kutengeneza tarehe 28.7.2008
wakimtumia kijana ambaye Dunia nzima inamjua.
Na Mungu anawaumbua, sasa
wanahaha, leo nitaongeza ushahidi kwenye mauaji ya haya.
Angalia
Mfano huu.
Tarehe 28.05.2008, JOHN
MNYIKA, akiwa mkurugenzi wa vijana CHADEMA taifa kipindi hicho, alitukutanisha
mimi Habibu Mchange, Marehemu Regia Mtema, Deus Mallya na vijana wengine
wawili, ofisini kwake ambapo kwa sasa ofisi hiyo inatumika kama ofisi ya Naibu
katibu mkuu, pamoja na mambo mengine tukajadiliana namna ya kulieneza Baraza la
Vijana na kuongeza wanachama wengi vijana, na tukapeana majukumu, kwamba mimi
nishuhulike mashuleni na vyuo vikuu vishiriki kama DIT na CBE, kwa kuwa
nilikuwa na mahusiano na watu wengi huko, DEUS MALLYA alipewa jukumu lingine
sambamba na marehemu REGIA MTEMA, lakini kwa pamoja tukawa kwenye kamati ambayo
mwenyekiti wetu ni JOHN MNYIKA mimi nikiwa mjumbe kutokea wilaya ya Temeke.
Tarehe 28.07.2008 usiku, CHACHA WANGWE aliuawa PANDAMBILI
DODOMA, na mtu aliyekuwepo kwenye tukio hilo ni DEUS MALLYA, nini kilitokea?,
Tarehe 29.07.2008 saa tano asubuhi, JOHN MNYIKA alifanya mkutano na
Waandishi wa HABARI, akimkana DEUSI MALLYA kwamba CHADEMA haimtambui, na kwamba
SERIKALI iwajibike kuueleza UMMA kwamba DEUS MALLYA ni nani na amewezaje kuwa
Dereva wa Chacha wangwe ambaye ni Mbunge huku chama kikiwa hakimtambui DEUS MALLYA
wala hakijawahi kumuona mahala popote na kwamba akamatwe Haraka na hatua kali
dhidi yake zichukuliwe Haraka.
Maana yake nini?. Ni kwamba MNYIKA na CHADEMA wamemkana DEUS
MALLYA kimkakati ili kukiondoa chama kwenye ushahidi wa mauaji ya kiongozi
wake mkuu msaidizi.
Jiulize maswali, kwanini
MNYIKA alimkana DEUS MALLYA aliyekuwa sio tu rafiki yake lakini mshirika wake
mkuu kwenye harakati za ujenzi wa chama?.
Kama hawahusiki Kumuua
WANGWE kwanini waogope kiasi cha kumkana mwanachama mwandamizi wao?.
Na kwanini Mbowe alitumia
nguvu kubwa sana kuhakikisha Deus Mallya anashinda Rufaa na anafutiwa Kesi?.
Na kwanini Mnyika na Mbowe
walimuomba Msamaha Deus Mallya baada
ya Kutoka Gerezani kwa kitendo chao cha Kumkana baada ya tukio la mauaji?.
Watanzania wanatambua kwamba MBOWE, LISSU, SLAA na CHADEMA
tumeshiriki kikamilifu kutengeneza matukio ya hatari yenye kuonyesha nchi
haitawaliki na upinzani hasa CHADEMA inanyanyaswa na Dola na polisi ili chama
kizidi kupata umaarufu wa kisiasa.
Hii ndio maana MBOWE na SLAA
wamemtuma kijana mmoja mrefu, mweupe mwenye mazoea ya kufuga nywele nyingi
aliyechanganya uraia wa Tanzania na German(ama nchi nyingine ya ulaya)(sitamtaja
jina kwa sasa. Mbowe na CHADEMA wanamfahamu) ambaye kwa sasa ni kiongozi katika
ngazi ya wilaya mkoa mmoja wa kaskazini kutekeleza mpango wa mauaji kwenye
matukio makubwa ya mikutano ya kisiasa hasa inayohusisha vurugu kati ya chadema
na polisi na kumuandaa mtu mmoja maalum kwa ajili ya kupiga picha matukio hayo
na kusambaza haraka mitandaoni huku mwengine akichukua VIDEO.
Kijana huyu ambaye ni
Swahiba wa MBOWE na LEMA, ameweza kutekeleza kazi yake hii Tarehe 05.2.2011
pale ARUSHA kwa kwaua watu kadhaa na kisha umma kuaminishwa kwamba mauaji yale
yalifanywa na polisi walipokuwa wanawazuia waandamanaji. Mpaka sasa polisi
inahangaika kujinasua kwenye matukio haya ya kutengeneza. Mimi, Mbowe,Slaa,
Lissu na Mnyika tunafahamu kila kitu.
Kijana Huyu kwa maelekezo ya
MBOWE kupitia kwa SLAA na MNYIKA ili kuwatisha wakazi wa IGUNGA, usiku wa
tarehe 9.9.2011 Wakitumia gari namba
T587 AZJ TOYOTA LANDCRUISER VX mali
ya FREEMAN AIKAEL MBOWE, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbunge wa Hai na Kiongozi mkuu
wa Upinzani Bungeni akiwa na HEMEDI SABULA, HENRI KILEWO na JOHN HECHE wakiwa
na vijana kadhaa wenyeji wa IGUNGA walimteka na kumtesa sana kijana MUSSA TESHA
na kisha kumpeleka Pori la MSITU
WA HANI HANI na kummwagia TINDIKALI
Usoni, ili eti vijana wengine waogope kuiunga mkono CCM na vyama vingine.
Na haya yote yalifanywa kwa
maelekezo ya SLAA na MBOWE na ndio maana baada tu ya Tukio, Slaa alimuagiza
mkurugenzi wa kampeni na uchaguzi aidhinishe malipo ili mkurugenzi wa fedha
alipe na vijana hawa wakapelekwa MWANZA na kuhifadhiwa kwenye Hotel ya MAGNUM kwa zaidi ya Mwaka mmoja.
Wakiendeshwa na Dereva mmoja maarufu sana wa chadema, sitamtaja kwa leo kwa
kuwa alikuwa anatii maelekezo ya viongozi wake.
Mauaji na Mateso yote ya
Kijangili yaliyofanywa IGUNGA na ARUMERU yaliwekwa kwenye mpango mkakati wa
CHAMA na kupitishwa na KAMATI KUU YA CHAMA.
Ni hatari sana kikao kikuu
cha chama kuhalarisha mauaji. Nimeambatanisha na sehemu ya ripoti na mkakati
huo wa mauaji.
U wapi sasa uzalendo wa
viongozi hawa?, uko wapi uzalendo wa mbowe, uko wapi uzalendo wa Slaa, Lissu na
wahuni wenzao wengine?. HAWA NI WAUAJI TU KAMA WAUAJI WENGINE. NA
WALAANIWE
MBOWE,
SLAA na LISSU, wanajua namna gani walivyomtuma muuaji wao
huyu aliyesomea kwa kushiriki kumuua mtu asiye na hatia pale morogoro tarehe 27.08.2012 ndugu ALLY ZONA aliyekuwa muuza magazeti pale msamvu, leo hii Dunia nzima
inajua kwamba Ally aliuawa na polisi, ila MBOWE,
SLAA na CHADEMA wanaujua ukweli halisi.
Wakati Dunia Nzima Leo
inaamini kwamba polisi wa F.F.U
walihusika kumuua David Mwangosi tarehe 2.9.2012
pale Nyororo Iringa, MBOWE, LISSU,
MNYIKA na SLAA wanaujua ukweli, wanajua ni namna gani mchezo huu ulipangwa,
namna gani mpiga picha aliandaliwa, namna gani taarifa za awali zilisambazwa na
namna gani mlipuaji alifika eneo latukio na kutekeleza kazi yake maalum na
baadae kuondoka kwa utaalamu wa hali ya juu, wanafahamu fika. Na kwenye hili
pia mpaka sasa polisi wanahangaika kujinasua, lakini bado wamekwama.
MBOWE,
SLAA, LISSU na CHADEMA huku wakishangilia, waliwaagiza vijana
wao wampige, na kumdharirisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ndani ya kikao cha kamati kuu Ndugu SHAABAN MAMBO tarehe 3.1.2014
ukumbini MBEZI GARDEN
CHADEMA
NI WATEKAJI.
Tarehe 6.1.2014. SLAA
aliwaagiza HEMEDI SABULA, MEDI,
MWAKYEMBE na REDBRIGADE kwenda
kufunga OFISI YA MWENYEKITI WA CHADEMA
TEMEKE JOSEPH YONAH , na ilipofika SAA
TANO USIKU wakamfuata mtaani kwake, wakamteka, wakampiga sana kisha
wakaenda kumtupa UNUNIO baada ya
kudhani kwamba wameshamuusa.
Na wakati wote wakimpiga na
kumtesa walisema wapo Tayari kumsamehe na kumuachia ikiwa tu atakubali kukiri
na kurekodiwa kwamba ametumwa na Zitto Kabwe, Mwigulu Nchemba, Usalama wa Taifa
kukihujumu CHADEMA. Jambo ambalo si
kweli na si sahihi.
Tulipomuokota UNUNIO
alipofika Hospitali, SLAA aliwatuma vijana wake kwenda kuiba PF3- na kwa njia
walizozijua mpaka sasa PF3 ya YONA ipo mikononi mwa SLAA ambaye kwa kweli ni
Muuaji na wala hana huruma.
SLAA akishirikiana na watesi
wenzake walimteka, kumtesa na kumjeruhi ndugu JOHN MARWA NYANCHABO,
kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 6.02.2014
mpaka tarehe 9.02.2014 na kumfungia
ndani ya chumba cha ofisi ya CHADEMA wilayani BAGAMOYO huku wakimlazimisha
kusema maneno ya hovyo kwamba ametumwa na CCM na ZITTO kuihujumu CDM na mambo
mengine.
Sasa kunihusisha mimi
naulipuaji wa helkopta ya Slaa na Mnyika helkopta ambayo waliopanda wana
utaalam wa ujangili ni kunikosea heshima. Na kwa kweli kwenye Hili Mwenyezi
Mungu wa Rehema atawalaani.
KUHUSU
MADIWANI KUHAMIA CCM.
Kuniambia kwamba mimi ndiye
niliyewashawishi wahame CHADEMA na wahamie CCM ili kisha wahamie ACT ni utoto ulipitiliza.
Pamoja na kwamba nina
mahusiano mazuri sana na Diwani SEBASTIAN PETER – OBAMA.
Ninafahamu kwamba OBAMA
alibakisha wiki mbili afukuzwe uanachama wake wa chadema, kama mnyika
alivyotangaza pale shinyanga,
Na ninafahamu kwamba OBAMA
ni miongoni mwa vijana wanaochukizwa na UBAGUZI wa wazi unaoendelea ndani ya
chama, na mimi nayeye uhusiano wetu umeimarishwa hasa na misimamo hiyo.
Hivyo ninakumbuka namna
ambavyo alikuwa anapambana kuhakikisha haki yake ya kutokufukuzwa inapatikana,
hii ni yeye na diwani wa kahama ndugu SHABAN BOBSON
Na hata alipojiunga na CCM
sikushangaa sana nilimpongeza kwa uamuzi wake kwa kuwa alikuwa kwenye political
frastruations nay eye ni muandishi wa hatma yake mwenyewe.
Kusema kwamba mimi
nilimshawishi ahamie CCM anaongopa, na anaongopa pengine anataka kuwaaminisha
kwamba viongozi wengi wa CHADEMA wana uwezo mdogo sana, kiasi kwamba wanaweza
kushawishiwa na mtu ambaye siyo mwanaCCM ili wao wajiunge CCM nay eye akabaki
kutokuwa mwanaCCM.
Lakini pia OBAMA anajaribu kuonyesha
namna ambavyo viongozi wetu wa upinzania wasivyokuwa na misimamo, kama jana
alijiunga na CCM na SLAA akatangaza hadharani kwamba huyo ni msaliti na kwamba
angefukuzwa muda mchache, leo karudi CDM anaitwa kamanda na mzalendo. Viongozi
wa namna hii ikitokea chama kikashinda dola wanaweza wakarubuniwa zaidi na
zaidi na kujikuta wanauza nchi kwa ahadi na matarajio ya kitoto
Lakini pia nina fahamu
kwamba OBAMA na mwenzake wapo kwenye UJIRA, wamelipwa ama kununuliwa wafanye
wanachokifanya ili kunjusuru uhai wa CHADEMA,
Na hili ni azimio halali la
kikao kati ya MBOWE, SLAA na viongozi wengine kilichoketi DODOMA wakati wa
Bunge la Bajeti, ambapo pamoja na mambo mengine, CHADEMA imeadhimia kuwanunua
viongozi na wanachama wote wanaowapinga. Tayari wamefanikiwa kwa OBAMA.
Leo hii Benson Kigaila
ametumwa na SLAA kigoma kununua viongozi wengine watoe matamko kama ya OBAMA,
na JOHN MREMA yupo TABORA anazunguka wilayani kugawa pesa ili waseme
watakayoyasema, Henry Kileo na Kigaila kwa pamoja wamemuhakikishia Joseph Yonah
wa Temeke kwamba iwapo atajitokeza hadharani kusema kuwa alikuwa anatumiwa na
ZITTO ama na CCM kupitia Mimi basi MBOWE na SLAA watabadilisha maisha yake na
kumuahidi donge nono. Tumefanikiwa kuwarekodi wakiongea ujinga huu.
Kwa hiyo sina shaka kwamba
madiwani hawa wanalipa walichokula, kwa hiyo ni wakati wao kuendelea
kubwabwaja, ukikubali kula cha mtu ukubali pia kuliwa.
Ila wawasaidie tu kuwaambia
watanzania kama yale waliyokuwa wanayalalamikia kutendeka ndani ya chadema siku
chache nyuma kama tayari yametatuliwa au bado?. Na kwamba Ufisadi wa mbowe
waliousema Tayari umeisha ama bado?, kwamba ubadhirifu wa SLAA waliousema
Tayari umekoma au Bado?, kwamba mauaji ya mbowe kumuua shelembi wa shinyanga
kama walivyosema yamebadilishwa ama bado?.
KUHUSU
LEKADUTIGITE NA NSSF
Kila mara Lissu amekuwa
akijitahidi kupambana na zitto hata katika maeneo asiyoyaweza.
Mimi habibu Mchange,
nimekuwa mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lekadutigite, kampuni iliyoundwa na
wasanii wa kigoma, na haijawahi kutokea hata siku moja zitto ama kampuni
kuhongwa pesa kiasi chochote na NSSF na kwamba Lekadutigite walitengeneza wimbo
ambao ni Tangazo linaloitangaza NSSF na kupewa milioni 21 kama gharama za
Tanzazo hilo na hili ni kwamba wasanii hawa walijitolea walipaswa kulipwa hata
milioni 900 kulinganisha na ukubwa wa kazi waliyofanya na ukubwa wa wasanii
husika, na maelezo mengine kuhusu malipo ya Nssf na lekadutigite tayari Nssf
wenyewe wameshayatolea ufafanuzi.
UNAFIKI WA LISSU.
·
Lissu anasema pesa za NSSF ndizo zilizotumika
kulipa hao madiwani. NI UWONGO – LEKADUTIGITE na NSSF mkataba wao wa kazi ni
January mpaka February 2013 na walikabidhi kazi kisha wakatumbuiza Arusha mbele
wa Makamu wa Rais
·
Niliacha kazi LEKADUTIGITE April 2013 ili
kuendelea na siasa hasa kuandaa jimbo langu la uchaguzi la kibaha mjini
·
Zitto na baadhi ya Viongozi wa CHADEMA
waligombana mwishoni mwa 2013 na mahakamani ni mwanzoni mwa 2014
·
ACT imeanzishwa mwezi may 2014, wakati hao
madiwani wameshaondoka kitambo CHADEMA
Kumuhusisha Zitto na mambo
haya ni kuweweseka kwa kiwango cha juu kwa watu hawa. Wao walishamfukuza zitto,
wakasema hana impact, sasa yanini wanahangaika naye?, kwanini hawalali
wanaweweseka naye?, kwanini wanajihami?, Hawajiamini?, kwanini wanakiogopa
kivuli chake?,
Waache kumfuata fuata na
waendelee na mambo yao.
Wajifunze kwa Zitto kukaa
kimya na kuendelea na Maisha.
Lissu namshauri aache
ubinafsi na ubabaishaji.
Dunia nzima inafahamu kwamba
alikula milioni 250 za wafadili kwenye shirika lao la kiraia na shirika likafia
hapo hapo nay eye kwenda kujenga ghorofa pale tegeta.
Lissu hawezi kuwa kama
zitto, zitto ni zitto na lissu ni lissu. Ninamshauri apunguze kukubali
kuchukuliwa kama zezeta.
LISSU ni MBINAFSI
ALIYEPITILIZA na UBINAFSI WAKE ndio umemfanya mpaka alipoombwa kushauri namna
bora ya kupatikana kwa wabunge wa viti maalum kama mwanasheria wa chama,
akaweka sharti na kuhakikisha kwanza Dada yake CHRISTINA LISSU anakuwa Mbunge wa Viti maalum, na ndio maana dada
yake alikuwa MBUNGE wa viti maalum wa chadema kwanza kabla ya kuwa MWANACHADEMA.
Alipelekewa kadi ya CHADEMA bungenidodoma baada ya kula kiapo cha ubunge.
LISSU NI MROPOKAJI
ALIYEKUBUHU, na wote mnafahamu namna alivyotumika kuropoka upuuzi kuhusu watu
na taasisi mbali mbali na sasa CHADEMA wanajifanya kuungana nao
Ni lissu ndiye ndiye
aliyemtukana na kumdhihaki Prof. BAREGU na kutaka ajitoe kwenye chama ama abaki
tume ya katiba kwa kuwa Tume haina weledi
Ni lissu ndiye aliyemzihaki
JOSEPH WARIOBA na kusema kwamba anaendesha tume ki CCM CCM na kwamba CHADEMA
haiungi mkono kitakachotolewa na Tume. – leo LISSU na CHADEMA wamekuwa
makwapani mwa TUME na WARIOBA
Aliwakashifu CUF akawaita
WAKE WA CCM, akawakashifu NCCR na MBATIA wao, akawakashifu MAASKOFU na MASHEIKH
akawakashifu wazanzibar. Leo aibu ya CHADEMA imefichwa na CUF na NCCR-MAGEUZI.
Aache kuwa mnafiki wa
kisiasa.
CHADEMA
INAKUFA KWA KASI
Mwisho,
Yanayoendelea kutokea kwenye
chadema leo ni kielelezo cha chama Kufa kwa kasi ya ajabu.
Watanzania tumewaongopea vya
kutosha sana, tumetengeneza matukio vya kutosha sana, na tumewalaghai
watanzania vya kutosha sana.
Sasa hakuna uwongo mpya
tunaoweza kuwapa, hakuna tukio jipya tunaloweza kulitengeneza, tumeamua
kujitekenya wenyewe halafu tunacheka wenyewe. Hii ni ishara ya kudidimia kwa
chama
Wazee wetu wanasema ukiwa
mwongo uwe na kumbukumbu, na ukitaka kuruka uagane na nyonga.
Kwa kuwa tulikubali kujenga
chama kwa kutegemea mtaji wa uwongo, na chama kimeamua kufa kwa kutumia uwongo
huo huo, mwisho wa siku jamii itatucheka kwa kuwazoesha uwongo.
Nitaendelea kusimamia kweli na
haki daima Dumu. Nitaendelea kulilinda na kulisimamia Taifa langu milele. Na
nitaendelea kupiganian demokrasia ya kweli kila siku
Mungu ibariki Tanzania
‘’SIO MAKOSA YANGU, MAKOSA
LABDA YA KAZI’’
Habibu
Mchange
0762178678/0658178678
‘’The Freedom Is Not Free’’